Aliyekuwa Mhamasishaji wa Klabu ya Young Africans, Haji Sunday Ramadhan Manara, amelishauri Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ kuelekea mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘CRDBFC’ utakaopigwa Mkoani Manyara, Juni 02, 2024.

Mchezo huo utakaozikutanisha Young Africans na Azam FC zote za dar es salaam umepangwa kupigwa katika Uwanja wa Tanzanite uliopo mjini Babati, Mkoani Manyara.

Manara amechukua nafasi kulishauri Shirikisho hilo la Soka kwa kuhisi Uwanja wa Tanzanite haukidhi kigezo cha kuwa mwenyeji wa mchezo wenye hadhi ya Fainali, tena unaozikutanisha timu zenye mvuto mkubwa nchini Tanzania.

Manara ameandika katika Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii: “NASHAURI TU. Kwa kilichotokea Arusha last weekend kinatupaswa kukifanya kama funzo, Semi final tu Washabiki walimwagika hadi wengine kukosa nafasi ya kuingia Uwanjani na hatimae kusababisha fujo.

“Ikumbukwe ilikuwa ni Sheikh Amri Abedi, Now tunakwenda kwenye fainali yenyewe ya Kombe la Shirikisho, tunaipeleka Babati Manyara, kiwanja chenyewe kina jukwaa moja tu, wataalamu wanasema capacity yake haifiki washabiki elfu tatu hadi elfu nne.

“Mamlaka zetu nawashauri kwa heshma kubwa ondoeni mechi pale kwa kuwalinda Washabiki, Babati ni Centre ya mikoa kadhaa inayoizunguka, Watu watatoka katika mikoa tofauti kuja kuona fainali na Yanga yao.

“Team hii ya Wananchi haijawahi kucheza huko toka iumbwe, imagine hamu ya Wanazi wetu kuiona Team yao, fikirieni na udogo wa uwanja, tunaweza kuepuka maafa kwa kuipeleka fainali sehemu nyingine.

“Kwa sisi watu wa Events na Promotions huwa tunazingatia vitu kadhaa kabla ya tukio husika, FACILITY, CAPACITY, CONIVNENCE NA LOGISTICS. Kwa Tukio kubwa la fainali kupeleka hapo hatukuzingatia mambo hayo.

“Najua pamoja na nia nzuri ya kuusambaza mpira maeneo mengi ya nchi lakini uwanja wa Babati haujawa tayari kuhost fainali hii kubwa, Wenzetu kote duniani fainali ya Makombe kama haya huchezwa katika Main Stadium ya nchi na hata Mgeni rasmi huwa kiongozi mwandamizi wa nchi.

“Kwa nchi za kifalme lazma aje Royal family kukabidhi kombe. By the way kibiashara pia sio sahihi kama tunataka tuumarket mpira wetu ndani na nje ya nchi, Imagine makampuni makubwa ya nje yakiona fainali katika uwanja kama huu watatuonaje?

“Watapata hamu ya kuja kuinvest kwenye mpira wetu? Nini nafasi ya Azam TV katika eneo la Production? Wanajisikiaje kurusha mechi ya fainali pale? Sponsor CRDB mileage gani watapata kwa fans wachache? Ahhh pengine mawazo yangu leo yanaweza kuwa sio sahihi.”

Viwanja AFCON kukamilika 2025
Wiki ya AZAKI: FCS, Vodacom Foundation wasaini makubaliano