Polisi wa Kaunti ya Kwale Nchini Kenya, wanamshikilia kijana mmoja anayeshukiwa kumnyonga hadi kumuua Bibi yake mwenye umri wa miaka 85, kisha kumuibia shilingi 300,000, ambazo alilipwa na Kampuni moja ya uchimbaji madini huko Kwale.

Mkuu wa Polisi Kaunti ya Kwale, Stephen Ng’etich amesema kijana (25), alikamatwa katika akiwa katika klabu moja ya burudani eneo la Kilulu na alikutwa akiwa na shilingi 270,000, ambazo alishindwa kuelezea alipozipata.

Wakati huohuo, mtu mmoja amefariki huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta wa jumba la kuhifadhi gesi huko Rabai kaunti ya Kilifi.

Kamanda wa polisi Kaunti ya Kilifi, Fatuma Hadi amesema mtu huyo amefariki wakati akipokea matibabu katika Hospitali ya Rabai, na chanzo cha ukuta huo kuanguka ni upepo mkali uliosababishwa na kimbunga laly.

Mlipuko Kiwandani wauwa 11 Mtibwa
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 23, 2024