Mratibu wa Maafa Mkoa wa Pwani, Rose Kimaro amesema takribani Watoto tisa wamezaliwa kwenye kambi za waathirika wa mafuriko ya Mto Rufiji Wilayani Rufiji na Kibiti, Pwani ambapo kati ya hao wapo mapacha wawili.

Kimaro ameyasema hayo wakati akizungumzia Maendeleo ya Waathirika hao, baada ya kupokea msaada wa nguo zenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 7, kutoka Umoja wa Wana Rufiji na Kilwa – UMARUKI.

Amesema, “Wamama sita wamejifungua na Watoto watatu wamezaliwa wilaya ya Kibiti na wengine Wilaya ya Rufiji, tunawashukuru Wahisani mbalimbali, Serikali kwa kutoa misaada mbalimbali ambayo inawasaidia Waathirika wa mafuriko kwa Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mafia.”

Akizungumzia hali ilivyo kwasasa, Mratibu huyo amesema mvua zimepungua na maji yanaendelea kupungua ambapo pia baada ya kutolewa kwa ushauri nasaha, baadhi ya Waathirika wamekubali kutoka kambini na kwenda kuungana na famila, ndugu na jamaa zao.

Wivu: Ngosha matatani kwa mauwaji ya mpenzi wake
Kilo 110 za Bangi zawaumbua wawili Tanganyika