Mkazi wa Goba Lastanza Kinondoni, Joseph Sanura maarufu kama Ngosha (31), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. kwa tuhuma za mauaji ya Penina Rwegoshora (28) mkazi wa Goba center.

Taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP. Muliro Jumanne imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Mei 23, 2024 majira ya 07:00 huko maeneo ya Goba Center, Kinondoni katika Pub ya iitwayo Penina.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uchunguzi wa awali wa Polisi unaonesha kulikuwa na mgogoro wa kimahusiano kati ya mtuhumiwa na marehemu kabla ya kushambuliwa kwa panga na mtuhumiwa.

Aidha, taarifa ambazo Dar24 Media imezipata kwa vyanzo mbalimbali zinabainisha kuwa Joseph alikua anamuhisi mpenzi wake anachepuka, na inasemekana siku hiyo Penina hakurejea nyumbani hali iliyomlazimu mtuhumiwa kumfuata ofisini kwake na kumshambulia hadi kupelekea umauti.

Inaarifiwa kuwa pia Penina ameacha watoto wawili na mwili wake unazikwa hii leo Mei 24, 2024 jioni huko Goba huku Polisi ikisema upelelezi
unakamilishwa ili mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka iwezekanavyo.

Aziz Ki aidengulia Young Africans
Watoto waliozaliwa kambi ya waathiriwa wa mafuriko wafikia tisa