Lydia Mollel – Morogoro.

Abiria 57 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Shabiby lenye namba za usajili T341 EEU kutokea Dar es salaam kulekea Dodoma, wamenusurika kifo baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kihonda kwa Chambo Mkoani Morogoro.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo hii leo Mei 25, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP. Alex Mkama amesema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kutaka kujaribu kuyapita magari yaliyo mbele yake.

“Kwa eneo lile haliruhusiwi kisheria ku overtake na tayari tuamshikilia Dereva wa basi kampuni ya Shabiby, Sadick Marugulu kwa kosa la kusababisha ajali iliyojeruhi watu 22 wa basi hilo na uchunguzi zaidi ukikamilika tutamfikisha Mahakamani,” amesema Mkama.

Kwa upande wa Daktari bingwa magonjwa ya dharula Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Nafsa Marombwa amesema majeruhi watano kati ya 22 hali zao si nzuri na wanaendelea kupatiwa huduma ya matibabu baadhi yao wakiwa wamevunjika eneo la mgongo.

Nao mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa basi hilo kuacha njia kwa kujaribu kuyapita magari mengine na kupinduka wakati akijaribu kukwepa bajaji hiliyokuwa mbele yake.

Hili ni tulio la pili ndani ya mwezi Mei, kwani  tukio la awali liliripotiwa Mkoani Morogoro Mei 14 iliyohusisha ajali ya Lori na Noah eneo la Mvomero na kusababisha vifo vya watu saba p na majeruhi Sita ambapo dereva wa ajali hiyo alikamatwa na Jeshi la polisi.

Shirima: Gari la Zimamoto halifiki eneo la tukio bila Maji
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 25, 2024