Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuteketeza dawa za kulevya aina ya bangi ekari 10 pamoja na kukamata maguni 80 ya dawa hizo na kusema litaendelea na operesheni ya kuwasaka wote waliokimbia na wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP. Justine Masejo imesema operesheni iliyofanyika Mei 26, 2024 katika maeneo ya Kisimiri Wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Aidha, amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuachana na biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo halito mwonea muhari mtu yeyote atakaye bainika kutumia pamoja na kujihusisha na biashara hiyo.

SACP Masejo pia amewaomba Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za baadhi ya watu wanaojihusisha na matumizi Pamoja bishara hiyo.

NBAA yajipanga kuendeleza utoaji elimu kwa Wananchi
Elimu ya fedha: Polisi Misenyi watakiwa kuwa mabalozi