Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara Nchini – TANROADS, umetakiwa kuhakikisha miradi yote ya barabara inayokamilika inapimwa ubora kwa kutumia vifaa maalum kabla ya Makandarasi kuikabidhi kwa serikali.

Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson wakati akifungua Maonesho ya siku mbili ya sekta ya Ujenzi nankusema mitambo na vifaa vya kisasa iliyonunuliwa hivi karibuni na TANROADS, itaisaidia Serikali kuondokana na changamoto ya kukabidhiwa Miradi ya Barabara iliyo chini ya kiwango.

Amesema, kabla ya hapo kulikuwa na matumizi yasiyoridhishwa ya fedha za walipa kodi kwani baadhi ya Makandarasi walikuwa wakikabidhi Barabara halafu mvua zikinyesha kipindi kimoja zinaweka mashimo na kufanya wabunge kuanza kutafakari namna ya kuishauri kwamba imejengaje barabara.

“Tatizo halikuwa ujenzi bali ukosefu wa teknolojia ya kupima udongo tangu mwanzo wa kazi lakini kwa sasa hali hiyo haitajitokeza na kuomba wataalamu kutumia teknolojia hiyo kupokea miundombinu iliyokamilika,” amefafanua Dkt. Tulia.

Kamati yapewa elimu ukokotoaji wa bei bidhaa za Mafuta
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Mei 28, 2024