Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amesema miundombinu ya usafirishaji kwa lango la Zanzibar haikidhi mahitaji ya sasa, kutokana na ukweli kuwa ilijengwa miaka ya nyuma wakati kulikuwa na idadi ndogo ya wasafiri.

Mrisho ameyasema hayo niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini, Plasduce Mbossa, wakati akifanya mahojiano na Dar24 Media na kusema shughuli za Bandari Nchini zimekuwa zikikua na kuongezeka, hali ambayo imechangia ongezeko la watumiaji wa usafiri na usafirishaji, tofauti na miaka ya nyuma.

Amesema, “ni kweli lazima tukiri kwamba ile miundombinu iliyopo pale ikilinganishwa na idadi ya abiria wanaopita haiwezi tena kudhibiti hiyo hali na kwa wasiofahamu ni kwamba Wataali wanapita kwenda kule, Viongozi wetu wanapita pale na hilo limeonekana na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari na tulianza kufanya matengenezo.”

“Ongezeko la watumiaji wa usafiri na usafirishaji ni tofauti na miaka ya nyuma hivyo kumewepo kwa abiria wengi wanaokadiriwa kufikia 5,000 hadi 8,000 kwa siku, ambapo idadi hiyo hufikia abiria hadi 10,000 kwa siku kwa kipindi cha sikukuu,” alifafanua Mrisho.

Hata hivyo, mesema si kweli kwamba mamlaka imeshindwa kusimamia utaratibu wa usafirishaji wa abiria kiasi cha kutokea kwa malalamiko kwa wasafiri wanaotumia lango la kusafiria Zanzibar na Bara, kwani Boti zinazofanya safari na idadi ya wasafiri hufahamika.

MALIMWENGU: Muziki wa ajabu wasababisha majanga
Mama Pinda Mwenyekiti mpya Shirikisho la amani - UPF