Magreth Kapungu mkazi wa Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro, amerejeshewa upya tabasamu lake, baada ya kupatiwa mahitaji kwa ajili ya matumizi kufuatia kukata tamaa ya kuishi kutokana na maradhi yaliyomuandama.

Tabasamu hilo, limerejeshwa na Mkaguzi wa Polisi, Dawati la Jinsia na Watoto mkoani Morogoro, Michael Rasha kwa Magreth ambaye ni ni mama wa mtoto mmoja (Robertson), baada ya kukata tamaa ya kuishi kutokana na kusumbuliwa na saratani ya koo ambayo iligundulika mwaka 2022.

 

Rasha alimkabidhi sabuni za unga, Sabuni za vipande, Unga, Sukari pamoja na Mafuta ya kupikia na kumpatia elimu juu ya ukatili, usalama na utoaji wa taarifa za uhalifu.

Aidha Mkaguzi Rasha ametumia wasaa huo kuwaomba wadau kujitokeza kumsaidia Binti huyo kutokana na ugumu wa maisha yake.

Serikali kutumia vikao rasmi kutoa elimu ya Fedha
OSHA watakiwa kuharakisha uchunguzi wa ajali Mtibwa Sukari