Hakuna sehemu Duniani ambayo haikosi mahala pa kutisha, lakini yanaweza kutofautiana kulingana na ukubwa wa vitisho vyenyewe ambavyo kila mmoja anaweza kuvichukulia kwa tafsiri yake na wengine wakaona ni kawaida kulingana na aina ya vitisho ambavyo wamewahi kukutana navyo katika maisha yao.
Maeneo ya kutisha mara nyingi huwa na historia na mizizi katika na tabaka za kitamaduni, ambayo inamaanisha kuwa yamehifadhiwa vyema kwa makusudi fulani, au ilibidi yawe hivyo kutokana na uhalisia na wenyeji hutoa simulizi husika ama kwa kukuonya usifike mahala hapo ama yamebaki kumbukumbu ingawa taswira yake hukupa uhalisia na kufanya mwili wako kusisimka kwa hofu au uoga.
Unachohitaji kujua ni kwamba kuna matukio yamewahi kurekodiwa katika sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo gereza la zamani la huko Mansfield, Ohio la Mansfield Reformatory, Ohio, wahenga wanasema kwamba inasadikika wafungwa wengi walikufa wakati wa vifungo vyao hapo zamani lakini mpaka leo wanaonekana wakiranda randa eneo hilo.
Gereza hilo halitumiki tena, kwani lilifungwa mnamo mwaka 1990 lakini unaweza kwenda kwenye ziara ya kuongozwa au ya kujiongoza kati ya Alhamisi na Jumapili mwaka mzima ukithubutu na bila kuhangaika utakutana na wafungwa hao wakiendelea na maisha yao ya kawaida, lakini unaonywa kuwa mtulivu wakati wote ili usidhurike.
Hadithi nyingine ambayo inashangaza ni ile ya kuhusu “kanisa la mifupa”. Takriban mifupa 50,000 ya binadamu imehifadhiwa katika nyumba hii ya watawa, ambayo imechukuliwa kuwa ni eneo la watakatifu na hapo zamani ilikuwa eneo maarufu la mazishi.
Lakini mifupa hiyo haiko kwenye lundo moja kubwa ambalo limeundwa kwa ustadi ikiwekwa vinara, mishumaa, vishika mishumaa, na zaidi bendera za maombi ya Wabuddha, ambapo mifupa pia hupigwa hapo juu katika muundo huo ulioanza 1870, wakati mtu wa ndani aliajiriwa kuchukua mifupa iliyohifadhiwa na kuigeuza kuwa sanaa.
Kingine kuna eneo lipo jiji kuu la Lomé huko nchini Togo, linaitwa Akodessewa. Ndilo soko kubwa zaidi la voodoo duniani, na si kwa ajili ya watu waliokata tamaa. Hebu fikiria kutembea kwenye vibanda na kukutana ana kwa ana na fuvu la kichwa cha binadamu au kichwa cha mnyama.
Watu wa Benin inasemekana kuwa mahali pa kuzaliwa kwa dini yao ya voodoo na huko New Orleans au Haiti wanaendesha soko kama hilo na wanaamini kwamba, ili kujiponya au kujiondolea laana hirizi zinaweza kukuunganisha na dawa inayofaa na ikakulinda na mabaya yote ya dunia, je unakubaliana nao?.