Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Wizara yake imeanza utaratibu wa kushirikisha sekta binafsi kwa utaratibu wa ubia (PPP), katika kutekeleza miradi ya miundombinu.

Bashungwa ameyasema hayo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma hii leo Mei 29, 2024.

Amesema, “ni katika kuipunguzia Serikali gharama kubwa za utekelezaji wa miradi ya miundombinu hasa barabara na madaraja ambayo Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha, lengo la kutumia utaratibu huu ni kujenga miundombinu na kuitekeleza kwa wakati.”

Aidha ameitaja iradi inayotekelezwa kwa utaratibu huo kuwa ujenzi wa barabara ya Kibaha-Chalinze-Morogoro-Dodoma (Expressway) yenye urefu wa kilometa 423.8 kwa mfumo wa kulipia.

Manyara: Watatu mbaroni kwa kutapeli Mamilioni
Mzee Kimbwembwe wa Magufuli atua na Jogoo Bungeni