Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameapa kupambana na rushwa kwenye Mkoa huo kuwatahadharisha Watumishi na viongozi wengine wenye kuendekeza vitendo hivyo akisema siku zao zimekaribia, huku akimsimamisha kazi Mganga Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Dkt. Petro Mboya na watumishi wengine wa idara ya Afya Wilayani humo.

Makonda ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara huko Ngaramtoni Jijini Arusha, baada ya kubaini kuwa Watumishi hao bado wanaendelea na kazi wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao juu ya ubadhirifu wa zaidi ya Shilingi Milioni 600, zilizokuwa zitumike kwenye sekta ya afya.

Aidha, Makonda pia amesema anestaajabishwa na Jeshi la Polisi Wilayani Arumeru kushindwa kumpata Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya Arumeru, anayedaiwa kutoroka kwa kuiba Shilingi Milioni 333 za serikali na kuwaambia Wananchi Halmashauri yao imeoza na inanuka rushwa katika idara mbalimbali.

Hata hivyo, amesema ataandika barua Serikali kuu kuomba kuongezewa nguvu kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Mkoani Arusha, ili kupambana na vitendo vya rushwa alivyosema vimekithiri kwenye Mkoa huo.

Rais Samia kufanya ziara ya kikazi Jamhuri ya Korea
Manyara: Watatu mbaroni kwa kutapeli Mamilioni