Anafahamika kama Thomas Fuller, Mtaalamu wa Hisabati wa Kiafrika anayejulikana pia kama “Negro Tom” na “Virginia Calculator”, alikuwa Mwafrika mtumwa aliyezaliwa Benin mwaka 1710 akijipatia umaarufu mkubwa kwa kwa uwezo wake wa kukukotoa hesabu mpaka akitwa jina jingine pia la kikokotoo cha akili.

Fuller alisafirishwa hadi Amerika kama mtumwa mwaka wa 1724. Kiukweli Fuller alikuwa na uwezo wa ajabu wa kuhesabu, akigunduliwa kipaji chake na Wanaharakati wa kupinga utumwa ambao walimtumia kama maonesho kwamba watu weusi walikuwa bora na si duni kuliko wazungu katika taaluma.

Taarifa zake zilienea kwa haraka na wakajitokeza watu ambao hupenda kuhakikisha mambo ili kujaribiu uwezo wake ambao ni Hartshorne, wakamuuliza kuna Sekunde ngapi ndani ya mwaka mmoja na nusu, kitu ambacho kilimchukua dakika mbili pekee kuwapa jibu lao kuwa Sekunde 47,304,000.

Hawakutosheka, kwani walimpa tena swali la pili wakimuuliza ni sekunde ngapi mtu mwenye miaka 70, siku kumi na saba na saa kumi na mbili atakuwa ameishi?bila kuchelewa ndani ya dakika moja na sekunde 30 aliwajibu kuwa mtu huyo angekuwa ameishi kwa Sekunde 2,210,500,800.

Kisha likafuata swali la tatu, wakimuuliza kuwa “tuseme mkulima ana nguruwe sita, na kila nguruwe ana nguruwe sita, mwaka wa kwanza, na wote wanaongezeka kwa uwiano sawa, hadi mwisho wa miaka minane, mkulima atapata nguruwe ngapi na katika dakika kumi, alijibu kwamba ni Nguruwe 34,588,806.

Safari hii alichelewa kidogo kwani tofauti ya muda kati ya kujibu kwake swali hili na maswali mawili ya awali, iliisababishwa na kosa dogo alilofanya kutokana na kutoelewa kwa ufasaha swali hilo, hivyo Hartshorne na Coates wakathibitisha kuwa uwezo wa Fuller kiakili ni lazima ungekuwa mkubwa zaidi.

Mtumwa huyu alifanya kazi kwa bidii katika shamba katika maisha yake yote na pia alikuwa akizungumza kwa heshima kubwa ya bibi yake ambaye anasema hakuwa tayari kumuuza, licha ya kuahidiwa kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa watu kadhaa waliokuwa wakinunua watumwa.

Mmoja wa watu hao, Coates baada ya kujionea hali halisi ya uwezo wa kiakili wa Fuller alisema mbele yake kwamba inasikitisha hakuwa na elimu sawa na fikra zake, lakini Fuller alimjibu akisema, “hapana, ni bora sikuwa na elimu, kwa maana watu wengi wasomi ni wapumbavu wakubwa.”

Ama kweli, akili ni nywele kila mtu ana zake. wakati msomi akisikitika kumuona Fuller hana elimu, yeye anaona wasomi ni wapumbavu, je? ni kwanini Fuller almaarufu kama Kikokotoo anaona kwamba wasomi wengi wana shida? hili ni fumbo kwani hakuhojiwa ili kutoa sababu zake ilo nikukaribishe kwa maoni juu ya hili utpe mtazamo wako. Hii ni Dar24 Media.

Dkt. Msonde: Madai ya Walimu yawasilishwe, yashughulikiwe
Ukarabati Mv. Magogoni kukamilika Desemba