Klabu ya Aston Villa inatajwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili Kiungo kutoka nchini England na Klabu ya Chelsea Conor John Gallagher, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya Kiangazi.

Gallgher anatajwa kuwa mbioni kuondoka Chelsea, kufuatia Uongozi wa Klabu hiyo kumweka sokoni kwa mkakati wa kusaka fedha zitakazotumika kusajili wachezaji wengine klabuni hapo, pamoja na kukwepa Kanuni ya Matumizi ‘FFP’.

Gazeti la Independent limeripoti kuwa Kocha Mkuu wa Aston Villa Unai Emery anapendezwa na uwezo wa Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, na tayari ameshaanza kuusukuma Uongozi wa juu kuhakikisha anaipata huduma ya Gallagher kuanzia msimu ujao 2024/25.

Gazeti hilo linaeleza: “Aston Villa wanaangalia uwezekano wa kumsajili Conor Gallagher ili kuimarisha kikosi chao kuelekea kwenye kampeni za msimu ujao, ambapo watashiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, huku Chelsea wakiwa tayari kufanya Biashara hiyo.

“Aston Villa inavutiwa na Gallagher, kufuatia Kocha Mkuu Unai Emery kuamini anaweza kuendana na mfumo wake. Tottenham Hotspur nao wanatajwa kwenye mbio za usajili wa Kiungo huyo, japo mipango yao haiko madhubuti kama ilivyo kwa The Villians.”

Kylian Mbappe kufumbua fumbo
Rage amng’ata sikio mwekezaji Simba SC