Tanzania imezindua Programu ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ya kuwasaidia Wanawake wa Afrika pamoja na Mkakati wake wa Kitaifa ikiwa na lengo la kuhifadhi mazingira katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza madhara ya kiafya, kupunguza mzigo wa mama na mtoto na ukatili wa kijinsia wakati wa kutafuta kuni na kuimarisha shughuli za kiuchumi na Kijamii.

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameyasema hayo jijini Luanda Nchini Angola akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko katika mkutano wa 42 wa Mawaziri wa Nishati na Maji wa Nchi za kusini mwa Afrika – SADC, ambapo aliwaomba Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo kuunga mkono juhudi hizo zilizoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha, pia alielezea umuhimu wa Matumizi wa Nishati safi ya kupikia na matumizi mengine kwa Nchi za Afrika huku akiishauri Sekretarieti ya SADC kutambua juhudi zinazofanywa na nchi wanachama katika kuendeleza program na miradi mbalimbali ya mafuta na gesi inayotekelezwa na nchi hizo na kuratibu katika utafutaji wa rasilimali fedha kama inavyofanyika katika eneo la Nishati ya umeme.

Mkutano huo wa Mawaziri ambao ulitanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu pamoja na wataalam ulijadili hali ya uzalishaji na upatikanaji wa umeme katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika, uendelezaji wa nishati ya mafuta na gesi pamoja masuala ya maji, ambapo Kapinga aliongozana na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mha. Innocent Luoga pamoja na Kamis

Mtuhumiwa wa mauaji, msafirishaji dawa za kulevya wanaswa Arusha
Mashirika ya ndege ya Kimataifa kutangaza utalii wa Tanzania