Swaum Katambo, Mpanda – Katavi.
Mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari St. Mary’s iliyopo Manispaa ya Mpanda, Luis Emmanuel (17), amefariki dunia baada ya  kunywa kemikali inayodhaniwa kuwa ni ethanol katika maabara ya shule hiyo akiwa na wanafunzi wengine wawili.
Katika tukio hilo, Luis alikuwa na Wanafunzi wenzake wawili wa kidato cha nne katika shule hiyo wakifanya usafi katika maabara ya kujifunzia masomo ya sayansi kwa vitendo iliyopo shuleni hapo, huku wakisimamiwa na Mwalimu John Mtafya ambaye alitoka nje kuendelea na shughuli nyingine za kimasomo.
Inaarifiwa kuwa Mwalimu huyo aliwaacha Wanafunzi hao wakiendelea na usafi na ndipo walipoingia katika chumba cha kuhifadhia Kemikali ambayo walichukua kemikali aina ya ethanol na kuinywa na baada ya kumaliza usafi waliendelea na masomo pasipo kusema chochote.
Wanafunzi wengine Evangelist Deodatus (20), mpaka sasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na Anastasia Zakayo (17), hali yake ni njema na anaendelea na masomo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni Mosi, 2024
Wazalishaji Vyakula vya Mifugo waonywa, sheria kuwakabili