Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Polisi Kata ya Bagara Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Selestine Mushi ametoa somo la kupinga ukatili na unyanyasaji kwa Watoto kwa Wananfunzi wa shule ya awali na Msingi ya Deira, iliyopo Mtaa wa Sawe Maisaka, Babati.

Polisi Kata huyo,  amewataka Wanafunzi hao kutofumbia macho matukio ya ukatili na badala yake watoe taarifa kwa Wazazi, Walimu na Kituo cha Polisi pale wanapoona dalili au matukio kama hayo, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni 3, 2024
Tanga: BRELA watoa elimu maonesho ya Biashara, Utalii