Rais wa Kenya, William Ruto amewataka Wananchi hasa Viongozi wa kisiasa kuacha tabia ya kueneza siasa za ukabila kwa manufaa yao binafsi na badala yake wahubiri amani kwa jamii.
Ruto amesema siasa za ukabila na ubabe hazina nafasi Katika taifa hilo na kusisitiza uhimu wa Wananchi kuungana kwa manufaa ya taifa, ili kujiletea maendeleo.
Wakati hayo yakijiri, Wakazi wa Hindi kaunti ya Lamu wameapa kuifunga barabara kuu Lamu-Witu-Garsen, ili kuzuia malori ya mizigo yanayotoka bandari ya Lamu kuelekea Ethiopia.
Wakazi hao wamesema hatua yao hiyo ni kuonesha ghadhabu zao baada ya kukosa ajira bandarini wakidai ajira zinatolewa kwa watu wasiokuwa wakaazi wa Lamu.

Dkt. Biteko: Watanzania tofauti ya Dini, Siasa isiwagawe
Waziri Mkuu ayakataa Mazombi Geita