Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwanammuziki maarufu nchini Korea, Cho Yong-pil, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii.

Cho ambaye yupo katika fani ya mziki kwa zaidi ya miaka 50, anaelezwa kuwa ni mmoja wa Wanamuziki nguli, wenye ushawishi mkubwa nchini Korea aliyeshinda tuzo mbalimbali kupitia kampuni ya YPC.

Cho ambaye ameimba nyimbo mbili kuhusu Tanzania, “Leopard of Kilimannjaro na Like Serengeti” alimweleza Rais Samia kuwa anaipenda Tanzania na anatamani kufika kwa mara ya pili, kabla hajaondoka duniani.

Rais Samia alimshukuru Cho kwa nyimbo zake hizo ambazo kutokana na umaarufu wake zimeitangaza Tanzania sio tu Korea bali duniani kote, na kumsihi arejee Tanzania, ili atunge nyimbo kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii na utamaduni.

Taasisi za Umma kufanya tathmini ya utekelezaji 
Agizo la Waziri Silaa laanza kutekelezwa