Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amemaliza ahadi yake aliyoitoa kwa Chama cha Mapinduzi – CCM, kwa kukabidhi boksi 150 za Marumaru alizoahidi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani.

Akizungumza Katika zoezi la kukabidhi Marumaru hizo katika ofisi za CCM Kibaha mkoani Pwani, Waziri Ulega amesema dhamana aliyopewa na Dkt. Samia ni heshima kubwa kwa Mkoa wa Pwani, hivyo hana budi kujitoa kikamilifu kukichangia Chama na kusisitiza kuwa ndicho kilichomlea tangia akiwa kiongozi wa Vijana wa CCM mkoani humo.

Amesema, “Ndugu zangu Wana CCM na Wana Pwani leo nafasi niliyonayo ni kwa sababu nimelelewa na CCM na kuonyesha nidhamu kubwa hivyo nakipenda sana Chama changu. Tutaendelea kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika hatua Kwa hatua hadi ofisi hizo zitakapokamilika.

Aidha Ulega ambaye awali alichangia boksi 50 na kufanya Jumla ya boksi 200, aliwaasa wale wote wanaoahidi kujitahidi kutimiza ahadi zao ili Ofisi hiyo mpya ya CCM iweze kumalizika na kuanza kutumika mapema iwezekanavyo huku Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Bernard Ghaty akimshukuru na kumtakia utendaji uliotukuka katika majukumu yake.

Naye Katibu wa Uchumi Kamati ya Ujenzi wa Ukumbi na Ofisi ya Chama ambaye pia Ni Mkuu Wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasri Ally amempongeza Waziri Ulega Kwa hatua hiyo na kuwaomba wadau wengine kumaliza ahadi walizozitoa Ili kufanikisha kumalizika Kwa Ujenzi huo.

Ajali ya Mbeya: 14 wapoteza maisha
Wakenya hawajatuzidi, ila wametuwahi: Idris Sultan