Boniface Gideon – Arusha.

Mkurugenzi wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata amesema kuna fursa nyingi za kiuchumi kwenye sekta ya Utalii endapo Vijana wataamua kuzichangamkia ambazo zinaweza kubadilisha maisha yao.

Florenso ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama KILIFAIR na kusisitiza kuwa wadau mbalimbali hususani Vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa za Utalii Nchini.

Amesema, “Vijana wachangamkie fursa za Utalii Nchini,na sisi tumeweza kuwekeza katika maeneo mbalimbali Nchini,hii inatoa fursa nyingi za ajira kwa Vijana wetu, tunatakiwa tuutangaze Utalii wetu wenyewe.”

Florenso ameongeza kuwa, Waandishi qa Habari nao wanatakiwa kuendelea kuihamasisha Jamii kutembelea vivutio vya Utalii, ili kuelimisha umma juu ya fursa zilizopo na Vijana waone umuhimu wa kusomea fani za Utalii.

Akizungumzia maonesho hayo, Florense amesema watayatumia kwa ajili ya kujitangaza na kubadilishana uzoefu hasa katika dunia ambayo walaji watumiaji wa huduma wamekuwa wakibadilika kutokana na mazingira yanayotokea duniani.

Ubovu wa Barabara: Wananchi wafunga njia Moro
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Juni 8, 2024