Lydia Mollel – Morogoro.

Jamii imetakiwa kujitokeza kuchangia damu na   kuachana na dhana potufu ya kuamini kuwa ukichangia damu mara moja unatakiwa kuchangia mara kwa mara kwani inasababisha uongezekaji wa damu mwili jambo ambalo sio kweli.

Hayo yamesemwa na Albert Malab Mtaalamu wa Maabara toka Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Albert Malabe hii leo juni 8, 2024 ambapo zaidi ya vijana 30 wa timu ya mpira wa miguu Morogoro Tanzanite Soccer Academy  wamejitokeza kuchangia damu kwa hiyari hili kuwasaidia wenye uhitaji mkubwa na waharaka.

“Kumekuwa na dhana hiyo kwamba mtu akichangia damu kwa mara ya kwanza inatakiwa kila baada ya muda huwe unachangia hili uzidi kuwa salama naweza kukanusha hilo sio sahihi kwasababu mwili wenyewe unajua kuwa mtu huyu hapa anatakiwa damu kiasi gani,” alisema Malabe.

Pia Malabe ameitaka jamii kuona umuhimu wa kuchangia Damu kwani kutawasaidia kutambua afya zao ikiwa ni pamoja na kutambua kama wana ungonjwa wa homa ya ini au maambukizi ya virusi vya Ukimwi na pia Wapo tayari kuwapokea watu wote watakaojitokeza na wakati wowote.

Naye Mtendaji Mkuu wa kituo cha Morogoro Tanzanite Soccer Academy, Boniface Kiwale  amesema hii sio mara yao ya kwanza kufanya hivyo bali wanautaratibu wa kujitokeza kila mwaka kuchangia damu kwani wanatambua uhitaji uliopo na pia ni wajibu wao kuisaidia jamii .

Ikumbukwe kuwa uchangiaji wa damu hauna madhara yoyote kiafya hivyo jamii ijitokeze kwa wingi kuhakikisha iinachangia damu hili kutokomeza vifo visivyo vya lazima vinavyosababishwa na ukosefu wa damu hospitalini.

Wasiojulikana wavunja madirisha ya Shule, wakimbia
Watanzania washauriwa kufanya utalii wa ndani