Boniface Gideon – Arusha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Bougainvillea Group of Lodges, Nico Ombay amewashauri Vijana kusomea masuala ya Sekta ya Utalii, kutokana na kuwa na uwanda mpana zaidi wa fursa za ajira Nchini.
Akiongea na Waandishi wa Habari hii leo Juji 8, 2024 kwenye maonesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama KILIFAIR, Ombay amesema pia amewashauri Watanzania kufanya Utalii wa ndani kwani una gharama nafuu.
Amesema, “nawaomba Watanzania tuupende Utalii wetu,tunavyo vivutio vingi sana ambavyo vitakufanya mtu ufurahie maisha,tuna ngorongoro na Serengeti na vivutio vingine vikubwa ambavyo vinavutia zaidi, kufanya Utalii kuna faida nyingi sana ikiwemo kuondoa msongo wa mawazo na kuimarisha Mahusiano na familia yako.”
Ombay ameongeza kuwa, kampuni yao pia imejipanga kufanya upanuzi zaidi wa uwekezaji na kuongeza uwanda zaidi wa ajira kwa Vijana.
“Sekta ya Utalii inanafasi nyingi sana za ajira kwa Vijana waliosomea mambo ya Utalii,hivyo niwaombe Vijana ambao hivi sasa wanasoma,basi wasiache kusomea masuala ya Utalii lakini pia kwa Wazazi wasiache kuwasomesha Watoto wao hasa wakihitaji kusomea masuala ya Utalii,” alisema Ombay.