Boniface Gideon – Tanga.
Usajili wa wanachama kidigitali katika Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga umepata msukumo mkubwa baada ya Jumuiya hizo kupokea simu janja mpya kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, Husna Sekiboko.
Simu hizo zimekabidhiwa na Mbunge huyo leo kwa Jumuiya hizo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la UWT, mkoani Tanga kilichofanyika katika ukumbi wa CCM jijini Tanga.
Mbunge huyo alikabidhi simu 10 kwa kila Jumuiya zenye thamani ya sh. 12 million ikiwa na lengo la kuongeza kasi ya zoezi la usajili wa wanachama wa CCM kielectronic.
Akikabidhi simu hizo Sekiboko alisema anatambua kuwa uwepo wa Viti Maalum unategemea sana ushindi wa CCM hivyo alisisitiza juu ya umuhimu wa kuongeza kasi ya usajili kidigitali wa wanachama wa CCM na Jumuiya zake.
Alisema utekelezaji huo pia ni kwa mujibu wa azma ya Dr Samia Suluhu Hassan ambaye ametaka kuona mabadiliko ambapo amewataka watendaji wa CCM na Jumuiya zake kwenda kwa wananchi na kuwaelimisha ili wakipende Chama.
Akizungumza baada ya kupokea simu, Katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga, Teresia Makiyao alisema kuwa simu hizo zitaongeza kasi ya usajili.
“Hadi Jumatatu walikwisha sajili wanachama 994 na alisema idadi hiyo ndogo imetokana na uchache wa vifaa hususan simu. “Simu zitaongeza kasi na tumeweka lengo la kila wilaya kusajili wanachama 500 kwa mwezi,” alisema Makiyao
Naye Kaimu Katibu wa Wazazi Mkoa, Urasa Moses Nanyaro amesema wana lengo la kusajili wanachama 7000 kila wilaya kwa.mwezi,” alisema Nanyaro.
Hata hivyo Katibu wa Jumuiya ya Wanawake UWT mkoa wa Tanga Aziza Kiduda alisema anashukuru Mbunge huyo kwa kutoa simu izo ambazo amesema zitaongeza kasi ya kusajili ambapo lengo la umoja huo nikusajili wanachama zaidi ya laki tatu kwa mwaka.