Mkurugenzi wa TANTRADE, Latifa Hamis amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha biashara kufunguka.

Amesema Tanzania ni sehemu salama ya uwekezaji hivyo amewakaribisha wakorea kuja kufanya uwekezaji kwenye biashara mbalimbali nchini Tanzania.

Amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Korea usaidie kukuza uchumi wa Nchi zote mbili.

Amesema watanzania wajitahidi kuchangamkia fursa katika sekta mbalimbali zikiwemo za Kilimo,Usafirishaji, Miundombinu.

Amesema Watanzania wanapaswa kushirikiana na makampuni ya Kikorea, ili waweze kujifunza kutoka kwao kwani nchi yao ipo mbele kiuchumi.

Aidha ameushukuru umoja wa biashara wa kimataifa wa Korea (Korta )kwa kuwaunga mkono na kusaidia kufanikisha maandalizi ya maonesho ya 48 ya Kimataifa ya biashara Dar es Salaam.

Matumizi akili Mnemba: Stem Park yawapa darasa Wanafunzi
Dkt. Jafo: Serikali imeweka mazingira wezeshi kibiashara