Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR – TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde amekutana na ujumbe kutoka shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID), ili kujadili mbinu bora za KKK.
Ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi wa ofisi ya Elimu USAID Tanzania, Dr Thomas LeBlanc na wamejadiliana mbinu bora za kujifunza na kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) zilizothibitishwa na tafiti.
Wajumbe wengine kutoka USAID walioshiriki ni Caitlin Tulloch Naibu Mkurugenzi Ofisi ya Mchumi Mkuu wa USAID Washington na Amelia McDonough.
Wengine ni Msimamizi Mkuu wa Tafiti Bunifu USAID-DIV, Rashmi Menon – Mtafiti Mwandamizi USAID-DIV (Washington) na Abbas Nsanzugwanko – Mtaalam wa Ufuatiliaji na Tathmini ofisi ya Elimu USAID.