Scolastica Msewa – Arusha.

Taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu “Foundation for Disabilities Hope (FDH) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Mozzah Mauly, Mkurugenzi Mtendaji, Maiko Salali na Wafanyakazi wa FDH, wametembelea ofisi za makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Arusha na kumkabidhi na cheti cha pongezi Kamishna wa Uhifadhi, Shirika Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Juma Kuji.

Cheti hicho, wamemkabidhi kwa kutambua mchango wa shirika katika kusaidia watu wenye ulemavu na makundi maalum katika jamii ikiwemo walemavu, wakilenga kudumisha uhusiano uliopo kati ya TANAPA na FDH pamoja na kujadili maswala mbalimbali juu ya watu wenye ulemavu ikiwemo Kampeni “Niache Niishi; Utalii Jumuishi” ambayo itahamasisha watalii kwenda hifadhi za Taifa.

Dhima ya Foundation for disabilities Hope ni kuhamasisha watu wenye ulemavu kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya utalii ambapo italisaidia Taifa kupata mapato ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan.

FDH pia wameipongeza TANAPA kwa kazi kubwa ya kusimamia maliasili za Taifa pamoja na kusaidia watu wenye ulemavu katika jamii ambapo Mkurugezi wa FDH, Salali amesema wanajivunia makundi ya watu yenye ulemavu kushikwa mkono.

Ziara ya kikazi: Rais Samia kuwasili Katavi
Dkt. Tulia, Rais Putin wajadili amani ya Mataifa