Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Khamis Abdullah Amekabidhi vifaa vya teknolojia vya kusaidia kupokea na kufikisha bidhaa za posta vilivyotolewa na mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Akikabidhi vifaa hivyo hii leo Juli 12, 2023 Jijini Dodoma amesema lengo ni kukuza uchumi wa Wananchi na Taifa kwa ujumla pamoja na kuwezesha shirika la posta kuwafikia Watanzania wengi zaidi Nchini na kuhakikisha maeneo ya mbali wananufaika na huduma hii.

“ Vifaa hivi vitaimarisha uwezo wa shirika kutoa huduma za ushafirishaji wa ufanisi na huakika kote ndani na nje ya Nchi, lakini pia kuimarisha mawasiliano ya watendaji,” amesema.

“Watumishi wenzangu kuwepo kwa vifaa hivi ndani ya shirika la umma kutaendana na maono ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu Dkt. Samia inayolenga kujenga uchumi wa kidigitali na unaoenda na kasi ya maendeleo ya teknolojia Duniani”.Amesema Abdullah

Hata hivyo amesema mashine hizo zitasaidia kuimarisha shughuli za usafirishaji na kuzalisha fursa za kiuchumi wa maendeleo katika Taifa.

“Mashine hizi zitasiadia sana shirika kuaminika zaidi kwa wateja na Mashine hizi zinabebeka, zinaweza kutumika Kama njia ya Mawasiliano kwa wafanyakaz na wateja wake,” amesema.

Zitaboresha uwezo wa huendeshaji na utoaji wa huduma na kukizi matarajio ya wateja na vigezo vya ubora wa kitaifa na kimataifa, na hichi ambacho tuna kifanya leo ndio tafsiri ya mifumo kusomana

Watumishi wenzangu tutaliona shirika la posta kutoa huduma bora za kisasa na pia kuchangia uchumi wa nchi kutanuka kwa viwango vya juu, na Lazima twende kwenye teknolojia zinazoibukia,” ,mesema Abdullah.

Ameongezea kwa kusema UCSAF imekuwa ikichochea uchumi wa maendeleo ya mawasiliano kwa Wote Nchini kupitia jitihada mbalimbali katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafanywa kwa ubora usio na mvutano wa kibiashara.

Ruto abariki kujiuzulu kwa Inspekta Jenerali wa Polisi
Ziara ya kikazi: Rais Samia kuwasili Katavi