Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Samia Suluhu Hassan amewaomba wazazi wote nchini kusimamia ipasavyo maadili na malezi ya watoto wao ili kuijenga Tanzania iliyobora pamoja na Chama cha Mapinduzi,kupitia jumuiya ya wazazi

Ameyasema hayo hii leo Julai 13, 2024 akiwa anafunga wiki ya wazazi iliyofanyika Mkoani Katavi wakati huohuo akiwa bado kwenye ziara yake ya kikazi pamoja na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.

“Jumuiya ya wazazi elekezeni nguvu kwa watoto wetu kwasababu hao ndio watakuja kua Viongozi wa Chama chetu na Serikali pia,Sio vizuri kuona watoto wetu wakitumia madawa ya kulevya na mambo mengine Yasiyofaa nawaomba tuwachunge pia huko mashuleni hata kama tuko bize na shughuli zetu ,Utandawazi usitupotezee maadili ya kitanzania ” alisema Dkt. Samia.

Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia, Biden alaani
Mpaka yote ya Nchi yetu ipo salama - Dkt. Samia