Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amejeruhiwa kwa risasi wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Butler huko Pennsylvania.

Trump, ambaye ni mgombea urais mtarajiwa kwa chama cha Republikan, alionekana kupatwa na jeraha katika sikio lake la kulia na  Maafisa wa ulinzi walimzingira ili kumpa usaidizi.

Hata hivyo, katika taarifa ya ofisi ya maafisa wa ulinzi wa rais ilisema  Trump yuko salama na alipata majeraha kidogo na alikwishahudumiwa katika kituo cha afya.

Tayari Rais wa Marekani, Joe Biden amelaani vikali shambulio la kutumia bunduki dhidi ya rais huyo wa zamani wa Marekani Donald Trump akisema halikubaliki.

Katavi haina matukio mengi ya kiuhalifu - Rais Samia
Wazazi wahimizwa usimamizi maadili, malezi ya Watoto