Shirika la Upelelezi la Marekani – FBI, limesema linachunguza jaribio la mauaji la Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump baada ya Mtu mmoja kufyatua risasi na iliyomjeruhi sikioni.

Tukio hilo la Jumamosi Julai 13, 2024 lilitokea wakati Trump alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Pennsylvania.

FBI limesema mtu huyo aliyeuwawa mara tu baada ya kufanya shambulio hilo, ametambuliwa kuwa ni Thomas Matthew Crooks (20), mkazi wa jimbo la Pennsylvania.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona akiwa na silaha kabla ya shambulio hilo na waliziarifu mamlaka, huku Polisi wakithibitisha.

Kwaheri Katavi: Rukwa wamsubiri Rais Samia
Maghala ya Chakula: Tanzania kufikia uhifadhi hadi tani Mil. 3