Mwenyekiti wa bodi ya Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Nchini – FEMATA, Yusuph Kazi ameiomba TAMISEMI iandae bei elekezi ya tozo kwa maeneo ya wachimbaji wadogo nchini na waisimamie itumike kutoza Wachimbaji wadogo wote nchini ili kuondoa tofauti za tozo kwa wachimbaji wadogo katika Kila Halmashauri nchini.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na Mwandishi wetu kuhusu maazimio ya mikutano iliyofanyika katika maadhimisho ya Wiki ya Madini mwaka 2024 yaliyofanyika jijini Dodoma hivi karibuni amesema bei hiyo elekezi ipangwe kutumiwa katika Halmashauri zote nchini.

Amesema Wachimbaji wadogo katika Halmashauri zote nchini wanafanya kazi zinazofanana kote lakini wengine wanatozwa tozo ndogo huku wengine wanatozwa tozo kubwa zaidi na kutoa mfano Halmashauri ya Chato ambayo huwatoza Wachimbaji wadogo tozo hadi shilingi milioni 5 kwa mwaka kiasi ambacho kinazidi hata kiasi cha kupata leseni katika Wizara ya Madini ni shilingi milioni 2.

“Tumekuwa tukilalamika huu ni mwaka wa tano pamoja na kukaa vikao kuwaelewesha kwamba tunahitaji kuchimba na tunalipa mapato mengine ya TRA lakini bado wamekuwa wakifunga vitaru vyetu huku wakijua kwamba kwenye Kila uzalishaji tunaozalisha tunalipa asilimia 0.3 Kodi ya service lev inayokwenda serikali kuu na Kodi zingine nyinyi zinazokwenda serikali kuu” alifafanua Yusuph.

Alisema, “ili tujue kabisa gharama ya kulipa kwaajili ya uwekezaji wa uchimbaji madini ni kiasi fulani ili kuondoa tofauti hizo za tozo kwa wachimbaji wadogo nchini waendelee na uchimbaji bila vikwazo vyovyote wafikie malengo waliyojiwekea ya mwaka 2010/2030 ya maisha ni utajiri na Madini ni utajiri”

Yusuph ameongeza kuwa kwasasa kuna Halmashauri zinatoza tozo ya50,000/-, laki 2/, laki 5, laki 6 na zingine hutoza hadi milioni 5 jambo ambalo hupelekea malalamiko miongoni mwa Wachimbaji wadogo nchini kwani wanaposhindwa kulipa migodi yao hufungwa na kuikosesha mapato Serikali pia.

Aidha aliishukuru Serikali kwa jitihada zilizofanywa na Serikali kwa kutatua kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili Wachimbaji wadogo nchini ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku ya kuto kuwaondoa Wachimbaji wadogo wenye leseni katika maeneo wanayochimba madini.

Yusuph aliitaja kero nyingine iliyoshughulikiwa na Serikali ni pamoja na Halmashauri nchini zisitoze tozo kubwa kuliko kiasi kilichopangwa kulingana na Sheria mama.

Kishindo kikuu Mpimbwe wakimkaribisha Rais Samia
Malalamiko bei elekezi: Rais Samia awakomboa Wakulima wa Mahindi