Raia wa Rwanda leo Julai 15, 2024 wanaamua hatma yao kwa kushiriki uchaguzi mkuu huku Rais aliye madarakani, Paul Kagame akitarajiwa l kupata ushindi wa kishindo katika azma yake ya kuwania muhula wa nne madarakani hadi 2034.
Katika chaguzi tatu zilizopita, Kagame ambaye aliwahi kushika nyadhifa za Makamu wa Rais na Waziri wa Ulinzi kabla ya kuchaguliwa na Bunge mnamo mwaka 2000 kuwa rais wa nchi hiyo, alishinda kwa zaidi ya asilimia 93 na safari hii anachuqnq na wagombea wawili pekee na wasio na ushawishi.
Amekuwa pia akiitangaza Rwanda nje ya nchi kwa kuandaa mikutano, kusaini mikataba ya udhamini na vilabu vikubwa vya soka vya kimataifa na kuonyesha kuwa Nchi hiyo ni kivutio kikuu cha utalii wa ikolojia.
Hata hivyo anakabiliwa na kasoro kadhaa, ambapo Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakipiga kelele juu ya ukandamizaji wa vyombo vya habari na wapinzani wa kisiasa.