Mbunge wa jimbo la Kivuu, Geophrey Pinda ameomba kituo cha Polisi cha Wilaya Mpimbwe mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyesimama eneo la Halmashauri ya Mpimbwe na kuzungumza na Wananchi njiani katika msafara wa ziara yake, akielekea Mkoani Rukwa.

Pinda aligusia changamoto ya Polisi ya umbali wa kutoka Makao Makuu ya Polisi ya Wilaya ya jimbo na aliona kuna haja yakuhitaji kituo cha Polisi cha Wilaya.

Akijibu ombi hilo, Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani, Hamad Masauni amesema Serikali tayari imeanza ujenzi wa makao makuu ya Polisi ya Wilaya hiyo na kilichobaki ni kuimarisha miundonmbinu.

Amessma pia watapanga Wafanyakazi katika kituo hiko huku akiahidi kuboresha vituo vyote vya kata vya Wilaya hiyo ambavyo vimejengwa na Wananchi na vingine vipya kuletwa.

Rais Samia aelezea jitihada za kuufungua Mkoa wa Katavi
Bustani ya Mnazi mmoja kuwa chachu ya Utalii