Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta amesema ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga, Matai Kasanga Port ulikamilika April mwaka huu 2024 na gharama zilizotumika mpaka ufunguzi ni Bilioni 150 ikijumuisha Ujenzi na ushauri.
Aliyassma hayo kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan hii leo Julai 16, 2024 kuzindua Barabara hiyo yenye urefu wa KM 107 kwa kiwango cha lami.
Hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo imefanyika katika eneo la Matai Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa ambapo Rais Samia amesema awali usafiri kutoka Bandarini ulikuwa ukichukua siku nzima lakini kwasasa wanatumia masaa mawili pekee.
Amesema, “Barabara hii inatuunganisha na nchi jirani za Zambia, DRC lakini pia Burundi maana yake ni kwamba tunakuta utendaji wa biashara, kazi iendelee kwa mkulima kazi iendelee, kwa mchimba madini kazi iendelee.”
Wakati huo huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pia ameweka Jiwe la Msingi la Uwanja wa Ndege wa Rukwa, ikiwa ni sehemu ya Ziara yake Mkoani humo.