Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Selemani Jafo amezitaka Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinanunua dawa za Viuadudu Ili kuweza Kuuwa mazalia ya Mbu wa malaria ili kuondokana na kutumia Fedha nyingi ili kuweza kununua Dawa za kutibu ugonjwa wa malaria.

Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake alipotembelea kiwanda cha Viuadudu kilichopo Kibaha Mkoani Pwani, ambacho kinatengeneza Dawa ya kuua mazalia ya Mbu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo nchini – NDC, Nicolaus Shombe ameeleza malengo ya kuanzishwa Kwa kiwanda hicho.

Katika Ziara hiyo, Dkt. Jafo ametembelea kiwanda Eneo la kamaka industrial ambalo litajengwa Viwanda miasita na baadae Eneo la Viwanda la Sinno Tan ambalo litajengwa Viwanda Miambili.

Rukwa: Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi shule ya Wasichana
Mapungufu kusaidia upatikanaji sheria mpya za Habari