Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametaka jamii ishirikiane katika kuwaibua Wanasayansi wanawake.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Julai 17, 2024 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Rukwa.

Amesema, “kwa maumbile wanawake ni wanasayansi kwa kujua vipaji vyao ndio maana shule hizi zimejengwa tuibue wanawake wanasayansi, kazi yenu watoto wangu nikusoma kwa bidii.”

Katika kufanikisha Mradi wa kutengeneza shule za Sekondari za Wanawake maalumu za Sayansi nchini, Serikali ilitenga kiasi cha Bilioni 106.6 na mpaka sasa imetumika kiasi cha Bilioni 104.4.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema Wanafunzi Wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi watapewa kipaumbele Samia Scholarship.

Samia scholarship ni mpango wa serikali ya awamu ya sita kuwafadhili wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita wenye ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi.

Waacheni wajifunze muda wao bado - Dkt. Samia
Rukwa: Rais Samia aweka jiwe la msingi ujenzi shule ya Wasichana