Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dokta Samia Suluhu Hassan amewataka wana CCM kuwaacha wengine waendelee kujifunza, kwani muda wao wa kuendesha dola bado.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Julai 17, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Laela iliyopo Wilaya ya Sumbawanga Vijijini Mkoani Rukwa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.

“Wengine waacheni waendelee kujifunza bado ni wachanga hao ni watoto wetu wa chama cha Mapinduzi muda wao wakuendesha Dola bado Kabisa,” alisema Dkt Samia.

Aidha, akiwa hapo Rais amewaomba Watanzania kuelekea uchaguzi wa mwisho wa mwaka wa Serikali za mitaa, ambao unakwenda kuchagua viongozi wa mitaa na vitongoji wachague viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kua kinawaletea maendeleo.

Ashikiliwa kwa kutengeneza, kusambaza Dawa feki za kulevya
Tuwaibue Wanasayansi Wanawake - Rais Samia