Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekumbusha na kuisisitiza jamii juu ya ulipaji wa kodi ambazo zinasaidia katika uendeshaji wa miradi mbalimbali nchini.

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Julai 18, 2024 wakati akiwasalimia Wananchi wa Tunduma akiwa Njiani kuelekea Dodoma Mara baada ya Kumaliza Ziara yake Mkoani Rukwa.

Amesema, “miradi yote ni pesa tunayoikusanya kwa njia ya kodi kwa njia ya Tozo, niwaombe pamoja ndugu zangu wafanyabiashara popote pale ulipo Lipa unachokilipa ili tujenge Taifa letu.”

Simbachawene: Marufuku kuwasumbua Watumishi
Ajali za Pikipiki: Wazee watakiwa kuwaonya Vijana