Mahakama Nchini Kenya imebatilisha marufuku ya maandamano iliyotolewa na Polisi katika mji mkuu wa Nairobi na maeneo jirani.
Polisi ilitoa agizo hilo likielezea hali ya maandamano hayo yanaleta ugumu kwa maafisa wa Polisi kulinda salama wakidai yameingiliwa na wahalifu.
Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita mwezi mmoja wa maandamano dhidi ya Serikali ambapo watu wapatao 50 wanadaiwa kuuawa na raia walipanga Maandamano Alhamisi Julai 18, 2024 katika jiji la Nairobi.
Yalianza kwa lengo la kupinga nyongeza ya ushuru lakini baada ya kuondolewa kwa nyongeza hiyo sasa raia wanamtaka Rais William Ruto ajiuzulu.