Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi – CCM (UVCCM), wakiongozwa na Mwenyekiti wa umoja huo Taifa, Mohamed Kawaida na katibu wake, Jokate Mwegelo leo Julai 19, 2024 wamepokea vifaa vya Kilimo vyenye thamani ya shilingi Milioni 200 kutoka kampuni ya uuzaji wa vifaa vya Kilimo China (AMEC).

Vifaa vilivyotolewa ni Mashine18 za kukoboa na kuchambua mchele, zenye uwezo wa kukoboa magunia 100 kwa saa 24 na Gari za Kilimo (Power tiller) 24.

Aidha, Mwenyekiti Kawaida amesema hatua hiyo ni uunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu hassan kupitia mradi wakuwawezesha Vijana kujenga kesho iliyobora, maarufu kama (BBT)

Bonanza la Michezo kufanyika Julai 20 - 28 Pemba
Simbachawene aleta mkakati Kilimo cha umwagiliaji Kibakwe