Hatimaye Rais wa Marekani, Joe Biden amethibitisha kuwa hatogombea tena uchaguzi wa rais unaotarajia kufanyika Novemba 2024, akihitimisha uvumi uliokuwa ukisambaa kuwa alikuwa akikabiliwa na shinikizo la ndani ya chama chake cha Democratic.

Biden ametangaza uamuzi huo hii leo Julai 21, 2024 akisema anajiweka kando kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo angekabiliana na hasimu wake Donald Trump wa chama cha Republican, ila atasalia kama Rais hadi pale muhula wake utakapokoma.

Amesema, “imekuwa heshima kubwa maishani mwangu kuhudumu kama rais wenu, ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi yangu mimi kukaa pembeni.”

Biden (81) alikuwa akikabiliwa na wito wa kusitisha kampeni tangu kufanyika kwa mdahalo dhidi ya Donald Trump wiki tatu zilizopita, ambapo alionekana kuwa dhaifu na mwenye hoja tata.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 22, 2024
Balozi Mbarouk amuandikia Spika barua ya kujiuzulu