Kiongozi wa upinzani Nchini Kenya, Raila Odinga amesema hatoshiriki katika mazungumzo ya kitaifa hadi fidia itakapotolewa kwa kila mwathirika wa ukatili wa polisi.

Odinga ameyasema hayo na kuongeza kuwa pia anataka kuondolewa kwa kesi zote zinazohusiana na maandamano, kuachiliwa kwa wote waliotekwa nyara na walioko gerezani.

Hatua hiyo inajiri ikiwa ni siku chache tangu Chama cha walimu nchini humo – KUPPET, kutoa siku saba kwa Serikali kutekeleza mkataba wao wa maelewano CBA, malipo fedha wanazodai, kuajiriwa kwa walimu wa JSS na walimu wanagenzi la sivyo wataingia katika mgomo.

Hivi karibuni Kenya ilikumbwa na maandamano raia wakimtaka Rais Ruto ang’atuke madarakani, wakimlaumu kwa uongozi mbaya, ufisadi na vifo vya dazani za waandamanaji wakati wa maandamano ya awali dhidi ya serikali wakipinga kuidhinishwa kwa muswada wa fedha wanaodai unamkandamiza mwananchi.

Ukaguzi vyombo vya moto: Polisi yapiga marufuku fedha taslim
Umeme wafika Kisiwani Chole kwa mara ya kwanza toka uhuru