Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali huku akiwaondoa katika baraza lake Januari Makamba, Nape Nnauye na Stephen Byabato.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Jerry William Silaa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akichukua nafasi ya Nape Moses Nnauye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Deogratius Ndejembi ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na  kabla ya uteuzi huu alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu na teuzi na tenguxi xingine ni kama inavyoonekana katika kiambatanishi hapa chini.

 

 

Silaa Waziri mpya wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 22, 2024