Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteuwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo, Balozi Kombo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italy.

Balozi Kombo anachukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa huku Cosato David Chumi akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Chumi anachukua nafasi ya Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye atapangiwa kituo cha kazi.

Uganda: Waandamanaji, Polisi watunishiana misuli
Uteuzi: Ndejembi amrithi Silaa Wizara ya Ardhi