Muda mfupi baada ya kuthibitisha kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais, Rais wa Marekani, Joe Biden amemuidhinisha Makamu wake Kamala Harris kuchukua nafasi yake ili kuwania kiti cha Urais wa Taifa hilo.

Biden kupitia chapisho lake la mtandao wa X zamani Twitter, amemchagua Harris kushika nafasi hiyo akiamini huo ni uamuzi bora zaidi na kuwataka Wanachama wa Democrat kumuunga mkono.

Ameeleza kuwa, “leo nataka kumuunga mkono kikamilifu na kumuidhinisha Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu. Wanademokratii – ni wakati wa kuja pamoja na kumshinda Trump.”

Kamala Harris mwenye umri wa miaka 59 alijitosa katika siasa baada ya kupanda vyeo na kuwa mwendesha mashtaka mkuu wa jimbo  California, ingawa hata matukio makuu ya tasnia hiyo.

Uteuzi: Ndejembi amrithi Silaa Wizara ya Ardhi
Silaa Waziri mpya wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari