Waratibu wa maandamano nchini Uganda wameapa kundelea na mipango yao ya kuandamana siku ya Jumanne Julai 23, 2024 licha ya katazo la Serikali wakisema kinachofikiriwa na Polisi ni tofauti na matarajio yao.

Waandamanaji hao, wanasema inawalazimu kufanya hivyo ili kupinga rushwa, huku Polisi ikisema maandamano yanapaswa kuandaliwa chini ya ruhusa yao kwa kuhakikisha kuwa hakutakuwa na vurugu na Rais wa Taifa hilo, Yoweri Museveni akisema wanacheza na moto.

Hata hivyo, mmoja ya viongozi wa maandamano hayo, Louez Aloikin amesema hawahitaji kibali cha Polisi ili kufanya maandamano ya amani, kwani ni haki yao kikatiba.

Hivi karibuni Shirika la kimataifa linalochunguza viwango vya rushwa na uwazi la Transparency International, liliiorodhesha Uganda kuwa ni miongoni mwa mataifa yenye viwango vya juu vya rushwa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Julai 23, 2024
Balozi Mahmoud Kombo Waziri wa Mambo ya Nje