Hukumu nyepesi ambazo zimekuwa zikitolewa Mahakamani, kwa washtakiwa wanaothibitika kufanya makosa ya ubakaji wa Watoto na Wanawake umelalamikiwa na Baraza la Shehia ya Wawi Chake chake Pemba ambalo limesema haliridhishwi.

Wakizungumza shehiani hapo, wamesema hukumu za Mahakama maalum za kupambana na udhalilishaji, zinawafaidisha wabakaji, jambo ambalo, linafanya matendo ya namna hiyo kuendelea kukithiri.

Wamesema, mwaka 2018 Baraza la Wawakilishi lilipitisha sheria kali kwa watakaotiwa hatiani kwa udhalilishaji, lakini Mahakimu wamekuwa hawaitumii ipasavyo.

“Mahakama ikimtia hatiani mshitakiwa kwa makosa ya ukatili na udhalilishaji, adhabu yake ni kuanzia kifungo kisichopungua miaka 30 au maisha, ingawa hakuna aliyetekelezewa adhabu hiyo,” alisema Mjumbe wa baraza hilo Aisha Mohamed Juma.

Amesema, “kama sheria imeshapitishwa kwamba, atakaetiwa hatiani afungwe kuanzia miaka 30, nini kinawatia hofu Mahakimu na Majaji wetu’’

Kwa upande wake mjumbe wa baraza hilo, Omar Haji Omar alisema, Serikali kwa upande wake, imeshaongeza adhabu kwa wabakaji, ili kukomesha vitendo hivyo, kwa bado kuna ukakasi wa matumizi ya sheria husika.

Maandamano Uganda: Wabunge watatu kufikishwa Mahakamani
Maambukizi VVU bado tatizo mashariki mwa Afrika