Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika yametajwa kuendelea kuongoza kwa kuwa na maambukizi zaidi ya Ukimwi, ambapo Watu milioni 20.8 wamekuwa wakiishi na HIV na 450,000 waliambukizwa kwa mwaka 2023.

Akizungumza mjini Munich kwenye mkutano wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Mkuu wa shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa – UNAIDS, Winnie Byanyima ametahadharisha kwamba bado hatua zilizopigwa ni dhaifu na ulimwengu upo nyuma katika kuyafikia malengo ya 2030.

Amesema, ukanda huo licha ya kuwa ni hatari kwa maambukizi lakini pia unatajwa kuwa ni moja ya maeneo yaliyopata mafanikio ya kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 59 tangu mwaka 2010.

Hata hivyo, Byanyima amesema takwimu za mwaka 2023 zinaonesha maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na vifo vimepungua kutokana na kuimarika kwa upatikanaji wa tiba kwa wagonjwa na waathiriwa.

Hukumu nyepesi kwa wanaobaka Watoto zalalamikiwa
Kisa mafuriko: Wapendekeza mji mkuu uhamishwe