Baraza la Maseneta Nchini Liberia, limependekeza kuundwa kwa mji mkuu mpya mbali na jiji la Monrovia kutokana na athari za mafuriko kuukumba mji huo mara kwa mara, wazo ambalo limepokelewa kwa shauku na shaka.
Kupitia Kamati ya pamoja ya Baraza hilo la Seneti, ilipendekeza kuundwa kwa mji mkuu mpya, wazo ambalo lilitolewa wakati wa mkutano wa kujadili tatizo linaloendelea la mafuriko ambayo yalitatiza shughuli za kiuchumi na utendaji.
Wamesema mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa kati ya mwishoni mwa mwezi wa Juni na mapema mwezi Julai 2024, yaliwaacha hivyo ni vema wazo lao likafanyiwa kazi kwa kuangalia hali ya kidiplomasia.
Mji mkuu huo wa Liberia – Monrovia, umekuwa ukikabiliwa na mafuriko kwa miaka kadhaa na kuleta athari kubwa kutokana na msongamano wa watu, mfumo mbaya wa maji taka na ukosefu wa kanuni uliopelekea ujenzi holela.